Mkongwe wa muziki kutoka nchini Marekani, P.Diddy hatahudhuria tuzo za Grammy za 2024, ifikapo Febuari, huku chanzo kikidai ni kutokana na madai ya unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa katika miezi michache iliyopita.
Kwa mujibu wa The Hollywood Reporter, mwakilishi wa staa huyo alithibitisha kuwa hatahudhuria sherehe hiyo mwaka huu.
Ikumbukuwe kuwa Albamu ya Diddy, The Love Album: Off the Grid, imeteuliwa kwa albamu Bora ya Maendeleo ya R&B, huu ni uteuzi wake wa kwanza kama msanii wa peke yake katika muda wa miongo miwili na Diddy amechaguliwa mara 14 na kushinda Grammys tatu katika maisha yake yote.