Na Frank Aman – Geita.
Bingwa mtetezi wa mashindano ya Mapung’o Cup 2024, Malindi FC kutoka Nyaseki, Kata ya Butobela, ameanza kwa kishindo safari ya kutetea taji lake kwa kuichapa Protelo Academy FC ya Mjini Geita bao 1–0, katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Soko la Jumatano, kijiji cha Nyakagwe.5
Malindi FC ipo Kundi D pamoja na Protelo Academy FC na Casablanca ya Kata ya Bukoli.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kocha wa Malindi FC, anayefahamika kwa jina la Mzuzu, alisema wameshiriki Mapung’o Cup 2025 kwa lengo la kulinda heshima ya timu hiyo ambayo mwaka jana ilifanya vizuri na kutwaa ubingwa.
“Tupo hapa kuhakikisha taji halitoki, heshima ya Malindi FC inabaki palepale,” alisema Kocha Mzuzu.
Mashindano ya Mapung’o Cup 2025 yamedhaminiwa na mdau mkubwa wa soka kutoka kijiji cha Nyakagwe, Pascal Mapung’o maarufu kama King Mapung’o, ambaye ameendelea kuwa chachu ya maendeleo ya michezo kijijini hapo.