YANGA SC WAZIDI KUKABIA KWA JUU, WASEMA HAWAJALIPWA MISIMU MITATU YA UBINGWA

Klabubya Soka ya Yanga, imesema imeona taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF kuwa inawadai bila kutoa ufafanuzi wa deni lenyewe na kwamba wao hawajawahi kulipwa fedha yoyote ya Ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa Misimu mitatu mfululizo, (2021/2022, 2022/2023 na 2023/24).

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga, imeeleza kuwa TFF wamekuwa wakishikila fedha za Ubingwa kwenye akaunti zao kila Msimu unapomalizika, huku wakifahamu ni makosa na ni kinyume cha utaratibu.

“Hakuna uthibitisho wowote wa kimaandishi kuonyesha kama TFF wamewahi kulipa fedha hizi za Ubingwa kwa Klabu ya Yanga. Ni aibu na fedheha na kumtia dosari mdhamini kuendesha mashindano bila kumlipa Bingwa kwa misimu mitatu mfululizo,” inaleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, Yanga inaeleza kuwa, “Tunaelekeza, dawa ya deni ni kulipa kwa wakati ikiwa ni haki ya mshindi na inampa heshima mdhamini wa mashindano. leleweke, ada za malipo ya wachezaji wa kigeni walizozisema kwenye taarifa yao hulipwa mwanzo wa msimu mpya na hela hizi za Ubingwa hutolewa Mwisho wa msimu.”

Klabu ya Young Africans imeeleza kuwa haijawahi kupokea taarifa yoyote rasmi kutoka TFF kuhusu kuwa na deni kwao, hivyo wanaendelea kusisitiza kulipwa pesa yao ya
Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB, kwa msimu wa 2023/24, ili waweze kucheza mchezo wa Fainali Juni 28, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *