Msanii wa muziki wa Afrobeat, Primeboy amekamatwa tena na Jeshi la polisi la Jimbo la Lagos.Kukamatwa kwa msanii huyo kunahusishwa na kifo cha Mohbad.
Punch aliripoti kuwa msanii huyo alikamatwa Jumanne asubuhi, Machi 12, wakati wa ziara yake katika Idara ya Upelelezi wa Jinai ya Jimbo huko Panti, Yaba, pamoja na shahidi, Ayobami Fisayo almaarufu Spending.
Mohbad alifariki Septemba 12 akiwa na umri wa miaka 27, katika mazingira ya kutatanisha ambayo baadaye yalizua hasira na maandamano ya mashabiki wakitaka uchunguzi wa polisi ufanyike na kufunguliwa mashtaka kwa waliohusika katika kifo chake.