Rais Samia Suluhu Hassan amesema kufikia Januari 2024 changamoto ya umeme Tanzania itapungua kutokana na Bwawa la Nyerere kuanza uzalishaji ambapo kinu cha kwanza kati ya tisa vilivyopo kitawashwa.
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora nchini (PMAYA) iliyofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijiini Dar es Salaam.
Aidha ameongeza kuwa kinu cha pili cha kufua umeme katika mradi huo kitawashwa lakini hakitozidi April 2024.