Wikiendi ya Jumamosi Desemba 16,2023 Jambo Media kwa mara ya kwanza wamefanya tamasha kubwa la kuwakutanisha wapishi wa Ugali na tamasha hilo limepewa jina la Ugali Festival ambalo lilikuwa na lengo la kumsaka bingwa wa kusonga ugali.
Mbali na hivyo pia Tamasha hilo lilikuwa na burudani kutoka kwa wasanii kama Bright, Best Nasso, Nyumbu Mnjanja na wengineo wengi.
Hii ni mara ya kwanza kufanyika Tamasha la aina hii nchini.