Mwanamuziki mkongwe Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Koffi Olomide ametangaza nia yake ya kujitosa katika siasa na anakusudia kuwania kiti cha useneta kwenye jimbo la Sud-Ubangi, kaskazini magharibi mwa Kongo.
Koffi Olomide alichaguliwa na Rais Felix Tshisekedi mwaka 2022 kuwa Balozi wa utamaduni wa Kongo.