Kinda wa Kaizer Chiefs auwawa kwa kupigwa risasi

Msakata kabumbu wa klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Luke Fleurs ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni wezimjini Johannesburg.

Fleurs alipigwa risasi usiku wa Jumatano wakati akijaza mafuta gari lake, kwenye mitaa ya mji huo.

Kinda huyo beki wa Kaizer Chiefs, alijiunga na timu hiyo mwaka jana na alitajwa kuwa “beki wa kiwango cha juu” mwenye “uwezo mkubwa wa kiufundi.” Kifo chake kimeombolezwa na mashabiki wa soka kwenye mitandao ya kijamii. Polisi wanachuguza tukio hilo la karibuni katika taifa linalokabiliwa na uhalifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *