Mahakama kuu Jijini Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha Maisha jela watuhumiwa wawili Linda Mazure, Mlativia, na Martine Pravince, Mlativia, kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya hydrchloride yenye uzito wa KG. 5.09.
Watuhumiwa hao walikamatwa na maafisa wa Polisi wakishirikiana na idara mbalimbali tarehe 17/04/2019 majira ya 15:45hrs katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere eneo la ukaguzi wa abiria wanaondoka kwenda maeneo mbalimbali.
Akisoma maelezo ya hukumu ya kesi namba EC No. 01/2023 JNIA/IR/38/2019, Jaji Zedekia Kisanya alisema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kuwatia hatiani watuhumiwa hao waliokuwa wakisafirisha dawa za kulevya kwenda nchini Warsaw Poland kwa tumia ndege ya shirika la Qatar mruko namba QR 1347 kupitia Doha.
Washtakiwa hao wamepewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu wa kusafirisha dawa za kulevya ambavyo ni kinyume na sheria za nchi.