Klabu ya Simba imetozwa faini ya Tsh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la mashabiki wake ambao wametambuliwa kwa msaada wa picha jongeo (video) zilizosambaa mtandaoni, kuonekana wakimwaga vitu vyenye asili ya unga katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Klabu ya Simba imetozwa faini ya Tsh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa za maji kiwanjani wakati na baada ya mchezo dhidi ya Azam.
Klabu ya Simba imetozwa faini ya Tsh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la mashabiki wake kuingia kwenye eneo la kuchezea baada ya mchezo dhidi ya Azam kumalizika na mkutano wa Wanahabari ukiendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.