Kenya wakimbilia Tanzania kununua mafuta

Madereva kutoka nchini Kenya wamelazimika kukimbilia nchini Tanzania kununua mafuta ya petroli na dizeli kutokana na unafuu uliopo nchini ukilinganishwa na bei ya kenya.

Madereva hao wa malori na magari ya umma na binafsi, wamevuka mpaka wa Namanga huku wafanyabiashara wa Kenya wanaouza mafuta katika eneo hilo wakilalamika kupungua kwa biashara kutokana na kuongezeka kwa gharama ya mafuta nchini humo.

Katika mpaka wa Namanga bei ya petroli kwa Tanzania inauzwa tzs 3,297 na dizeli ikiuzwa tzs 3,343 huku bei ya petroli na dizeli kwa kenya ikiuzwa zaidi ya 3,400.

Aidha, wauzaji hao wameshangazwa na unafuu wa bei za mafuta nchini Tanzania licha ya tatizo hilo kuwa janga la kidunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *