Shirikisho la Soka Nchini (TFF), limesema kuanzia msimu ujao kutakuwa na mshirika wake maalum katika ubashiri wa michuano yote, ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa Taarifa ilitotolewa hii leo Mei 12, 2023 na Ofisa Habari na Mawasiliano, TFF, Cliford Mario Ndimbo imeeleza kuwa Mshirika huyo atashikilia haki hizo kwa kipindi chote cha makubaliano.
“Hivyo, yeyote mwenye nia au kuhitaji odds kwa ajili ya mechi ambazo zitakuwa chini ya TFF atalazimika kuwasiliana na mshirika huyo. Makubaliano yetu na mshirika huyo yatakuwa ni kwa ajili ya odds tu, na si ushirika mwingine na kampuni za michezo ya kubashiri kama udhamini au ushirikiano, iliezeza taarifa hiyo.
Aidha, taarifa hiyo pia imeeleza kuwa utaratibu huo ndiyo unaotumika katika Ligi mbalimbali barani Ulaya na kwamba hatua hiiyo ya TFF pia itazinufaisha kimapato klabu ambazo mechi zao zitakuwa zimeingia kwenye odds.



