Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Marufuku kuchimba dhahabu kipindi cha mvua

Kutokana na matukio ya wachimbaji wadogo wa madini mkaoni Geita kufukiwa na vifusi wakati wakichimba madini kujirudia kila mara, jeshi la polisi mkoani humo limewataka wachimbaji wadogo wote kuacha kufanya shughuli za uchimbaji hasa kipindi hiki cha mvua na badala yake wasubiri mvua ziishe ili kuepusha maafa yanayojitokeza.

Rai hiyo imetolewa na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita ACP Safia Jongo wakati akizungumza na Jambo Fm ofisini kwake juu ya mstakabali wa kudhibiti matukio ya wachimbaji wadogo kufukiwa na vifusi na kupoteza maisha hasa nyakati za mvua amesema sababu kubwa ya matukio hayo ni wachimbaji kutokufata sheria na kuchimba maeneo yaliyokatazwa .

Kamanda Jongo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa mkoa wa geita kuchukua tahadhari kwa watoto hasa kipindi hiki cha mvua kwa kuwalinda ipasavyo kutoakana na watoto wengi kupenda kuchezea maji hasa kwenye madimbwi hali ambayo inasababisha watoto kuzama na kusababisha maafa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *