Mtandao wa Fox News umebainisha kuwa maafisa wa polisi waliofika nyumbani wa rapa mkongwe P.Diddy na kufanya msako, wamefanikiwa kukuta kamera za siri kwenye moja ya nyumba za staa huyo.
Inaelezwa kuwa kamera hizo zimekuwa zikirekodi matukio kadhaa ikiwemo sherehe anazofanya kwake na kutumia video zake kuraghai watu maarufu/matajiri punde wanapokuwa wamekosana (Blackmail)