Mahakama ya Mjini Durban, Afrika Kusini imeendelea kusikiliza kesi ya mauaji ya rapa Kieran ‘AKA’ Forbes na rafiki yake Tebello ‘Tibz’ Motsoane, leo Machi 27, 2024. Ambapo licha ya washtakiwa watano wa mauaji hayo jina jipya limejitokeza ambalo ni la mfanyabiashara aitwaye Sydney Mfundo Gcaba.
Upande wa Mashtaka kupitia Wakili wa Serikali Elvis Gcweka alipokuwa akisoma hati ya kiapo ya Afisa mpelelezi, katika Mahakama ya Durban amesema mshtakiwa namba nne, Mziwethemba Gwabeni, alipiga simu kwa namba inayohusishwa na Gcaba, siku moja baada ya Forbes na Motsoane kuuawa na kiasi cha R803 455, ambacho sawa na Tsh/= 108,475,925.53 ziliamishwa kwenye akaunti ya benki ya mwombaji (Gwabeni).
Hata hivyo taarifa ya benki iliyoambatishwa katika hati yake ya kiapo haionyeshi muda wa miamala hii, anasema Gcweka.