Staa wa muziki kutoka nchini Marekani, Bruno Mars ametajwa kudaiwa deni la kiasi cha dola milioni 50, kwenye moja ya kasino za kamari huko Las Vegas.
Mars amekuwa akiishi Las Vegas tangu mwaka 2016 baada ya kusaini ushirikiano wa miaka mingi na MGM Resorts. Inaeleza kuwa staa huyo ameingia kwenye deni na kampuni ambayo alikuwa inamlipa iliatumbuize.
Kwa mujibu wa NewsNation, hasara ya kamari ya Mars imekuwa kubwa na amekuwa na deni kubwa kuliko kile anacholipwa.