Dereva wa gari la abiria aliyekuwa akiwaendesha Jonathan Majors ambaye ni muigizaji wa filamu na aliyekuwa mpenzi wake Grace Jabbari ametoa ushahidi wake hapo jana Mahakamani.
“Majors alijibu kwa jeuri wakati Jabbari aliponyakua simu yake kutoka kwenye mkono wake baada ya kuona ujumbe kutoka kwa mwanamke mwingine walipokuwa wameketi kwenye kiti cha nyuma cha gari, na hivyo Grace akaanza kumshambulia mwenzake” ameeleza shahidi huyo.
Hata hivyo Grace anadai alifanya hivyo baada ya kuona ujumbe tata kutoka kwa mwanamke ambaye alimwandikia mpenzi wake ““Laiti ningekuwa karibu ningekubusu.”