Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CPA Amos Makalla ametangaza kuwa ujenzi wa jengo la abiria uwanja wa Mwanza utaanza mapema mwezi Februari 2024 ikiwa ni baada ya taratibu za awali kukamilika.

Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo tarehe 12 Desemba, 2023 Jijini Dar es Salaam baada ya kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa Mkoa wa Mwanza na Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege( TAA). Halikadhalika, kikao hicho pamoja na mambo mengine kimejadili kumalizika kwa mgogoro wa uvamizi wa uwanja ndege na kurekebisha jengo la mizigo ili kuwezesha wasafirishaji wa minofu ya samaki kutumia uwanja huo.
Aidha, Mkuu wa mkoa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo na kuidhinisha fedha shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi jengo la Abiria.
Kiu ya uwanja wa Ndege wa Mwanza kuwa wa Kimataifa inakwenda kukamilika hivi katibuni kwani kwa mujibu wa ratiba, Mkandarasi anatakiwa kukamilisha ujenzi huo Mwezi Agosti 2024.