Msanii wa filamu Lupita Nyongo anatarajiwa kuongoza baraza la majaji katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la Berlin ifikapo Februari 2024, na atakuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya mtu mweusi kuongoza Baraza hilo.
Tamasha hili la 74 la Berlinale, linatajwa kuwa tamasha kubwa la filamu kwa Ulaya na kwa mwaka, ambalo litaanza Februari 15-25.