‘Jeshi la polisi bado mnabambikiza kesi’

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema bado anapokea malalamiko ya tatizo la Watu kubambikiwa kesi na Polisi na amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi aendelee kudhibiti vitendo hivyo.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 4, 2023 katika hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam.

“Bado napokea vikaratasi vya tatizo la kubambikiwa kesi Vituo vya Polisi naomba hilo pia mlitupie macho, wimbo wa Polisi mzuri sana na leo asubuhi kabla sijaja hapa niliufungua kwenye Youtube nikausikilizaa kisha nikaangalia Jeshi langu nikasema ingekuwa yanayoimbwa yote ndio yanayotendeka tungekuwa na Jeshi la Malaika”

“Mwakani tuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa nataka Jeshi la Polisi liwe makini kusimamia haki na kuhakikisha chaguzi zinakwenda kwa njia ya usalama”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *