Camera kufungwa barabarabi kukomesha rushwa

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo September 04,2023 amefungua wa kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania Jijini Dar es salaam ambapo amesema Serikali imejipanga kuboresha mifumo ya teknolojia ikiwemo kufunga camera barabarani ambazo zitasaidia kumaliza vitendo vya rushwa kwa Maaskari.

Rais Samia amemwomba IGP kukaza buti ili Jeshi linyooke hususani upande wa maadili, kwani yapo masuala bado Wananchi wanalalamika ikiwemo rushwa kwa baadhi ya Askari hususani Trafiki .

Aidha rais Samia amesema kuwa Wakati mwingine ni ngumu kurekebisha tabia lakini tabia itarekebishika kukiwa na teknolojia inayolazimisha Watu wafuate teknolojia inavyotaka akatoa mfano wa kuweka camera barabarani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *