Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Jambo Food Products kampuni pekee kutoka Tanzania iliyoshiriki  warsha ya kimataifa nchini Kenya

Kampuni ya Jambo Food Products imekuwa kampuni pekee inayojihusisha na uzalishaji wa vyakula na vinywaji kutoka Tanzania iliyochaguliwa na kushiriki warsha ya kimataifa ya siku tatu iliyofanyika kwa lengo la kuwezesha mwingiliano wa moja kwa moja kibiashara kati ya Makampuni ya Kibarazil na mashirika tarajiwa katika uwekezaji nchini Kenya.

Warsha hiyo iliandaliwa na Baraza la Brazili la kuagiza na kusafirisha kwa Makampuni ya Biashara(CECIEX), Shirika la Kukuza Biashara na Uwekezaji la Brazili (Apex Brasil) na Wizara ya Maendeleo,Idara na Huduma chini ya Mradi wa Ugavi wa Brazili kwa Usaidizi kutoka kwa Chemba ya Biashara ya Sao Paulo warsha ya Biashara ya Kiserikali ya Brazili imefanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Februari , 2024 katika Kempiski, Nairobi Kenya.

Kupitia Warsha hiyo ambayo Kampuni ya Jambo Food Products imewakilishwa na Bw.Mussa Rioba miongoni mwa fursa zilizopatikana ni pamoja na kufanya mikutano ya majadiliano ya kibiashara miongoni mwa kampuni za kibrazil ili kubadilishana uzoefua wa kibaisahara na fursa za kiuchumi na nchi zilizoshiriki kutoka barani Afrika ni   Kenya , Tanzania, Rwanda na Ethiopia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *