Migogoro Mikubwa Iliyompokea RC Mndeme Manispaa ya Shinyangaywarapiort1


Migogoro ya ardhi,usalama barabarani,kutokamilika kwa wakati kwa ujenzi wa soko kuu la Manispaa ya Shinyanga,bei ya sukari na mdororo wa bei ya pamba na chamgamoto ya nishati ya Umeme ni miongoni mwa changamoto zilizotawala katika siku ya kwanza ya ziara ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliyoifanya kwa na lengo la kupokea,kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika mkoa huo.


Akiwa katika viwanja vya kituo cha mabasi soko kuu katika Manispaa ya Shinyanga Februari 28,2024 mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mh.Christina Mndeme baada ya kusikiliza kero hizo amesema umeme si anasa na hivyo kuliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)mkoani Shinyanga kuhakikisha linapeleka umeme katika eneo la Nyanhende kabla ya Mwezi Aprili mwaka huu ambapo kuna malalamiko ya wananchi kutopatiwa huduma hiyo licha ya nguzo za umeme kupelekwa.


Kuhusiana na bei ya sukari,RC Mndeme amesema bei elekezi iliyotolewa na serikali ni kuanzia shilingi 2,800/= hadi 3,000/= kwa kilo moja na si vinginevyo na kufafanua kwamba serikali inaendelea kuchukua hatua kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari na kupandisha bei ya sukari.


Aidha amemagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Kuhakikisha ujenzi wa soko kuu la Manispaa hiyo kuhakikisha ujenzi wa soko hilo unakamilika ifikapo Mei 30 mwaka huu.


Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi kupitia mkutano huo amesema la polisi linaendelea kuchukua hatua kwa madereva wa mabasi wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *