Mahakama kuu ya Tanzania inayoshughulikia makosa ya rushwa na uhujumu uchumi iliyoketi katika masijala ya Shinyanga leo Septemba 7 2023 imeahirisha kusikiliza mashahidi upande wa Jamuhuri katika kesi no 3 ya uhujumu uchumi na ugaidi ya mwaka 2023 inayowakabili watuhumiwa 8 waliokamatwa mwaka 2017 wilayani kahama kufuatia mmoja wa mawakili wa upande wa utetezi kutofika mahakamani .
Katika kesi hiyo washitakiwa wote 8 wanakabiliwa na makosa 6 ya ugaidi ikiwa ni pamoja na kupanga njama ya kufanya vitendo vya kigaidi, kuajiri watu kwa ajili ya kufanya ugaidi huku mshitakiwa namba 2 na namba 8 wakikabiliwa na tuhuma za kufadhili fedha ambazo zingetumika katika vitendo vya kigaidi na mshitakiwa namba 1 na namba 8 wakikutwa na hatia ya kushiriki vikao vinavyohusishwa na vitendo vya kigaidi wakati wakijua ni tishio kwa umma.
Watuhumiwa hao wote ni wakazi wa Kahama na kesi itaendelea tena Septemba 8 2023 kwa kuwasikiliza mawakili upande wa Jamuhuri.