Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Homera aingilia kati wanafunzi kulazwa darasani

Mkuu Wa Mkoa Wa Mbeya Juma Homera Amemuagiza Afisa Elimu Mkoa Kumchukulia Hatua Za Kinidhamu Mwalimu Wa Shule Ya Sekondari Loleza Jijini Mbeya Sabina Haule Kwa Kosa La Kuwalaza Wanafunzi Wa Kidato Cha Sita Darasani Kwa Kile Anachodai Kuwa Ni Watukutu.

Homera Amesema Mwalimu Huyo Alifunga Bweni La Wanafunzi Hao Na Kisha Akawaamuru Kulala Darasani Kwa Makusudi Na Kisha Akaondoka Na Ufunguo Pasipo Kujali Hali Ya Kiafya Ya Wanafunzi.

Hata Hivyo Homera Amemtaka Mwalimu Huyo Kuwa Na Utu Kwa Wanafunzi Ambao Wazazi Wao Wamewapeleka Shuleni Hapo.

Kwa Upande Wake Mkuu Wa Shule Ya Sekondari Loleza Amesema Mara Baada Ya Kupata Taarifa Hiyo Alianza Kufanyia Kazi Kwa Ajili Ya Kutatua Suala Hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *