Klabu ya Yanga SC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji Jonas Mkude ‘Nungunungu’ kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Simba SC kufikia ukomo.
Mkude (30) raia wa Tanzania amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuwatumikia Wananchi mpaka Juni 2024.