Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Hofu Yaongezeka Gaza,Watu 120 000 Wakipoteza Maisha

Kadri vita ivyozidi kushika kasi ukanda wa Gaza, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Volker Türk hii amelaani mashambulizi aliyoita ya ‘kutisha’ yanayofanywa na Israel kwenye eneo hilo lililozingira, huku akirejelea wito wake wa muda mrefu wa sitisho la mapigaon na kuachiliwa huru kwa mateka wote waliosalia.

Akihutubia ufunguzi wa mkutano wa 56 wa baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi, Bwana Türk amesisitiza kuwa hofu inayozidi kuongezeka kila uchao ya vitendo vya uhalifu wa kivita huko Gaza vilivyoripotiwa na ofisi yake kuwa vimetekelezwa na pande zote mbili za mzozo huo uibuke tarehe 7 Oktoba 2023 kwa kuchochewa na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na Hamas dhidi ya Israeli.

Mpaka sasa Watu laki moja na Elfu Ishirini wameuawa,wengi kati yao ni  wanawake,Watoto na mauaji hayo ni  yale yaliyotokea kati ya Oktoba 7 hadi sasa kwenye eneo lililozingirwa Gaza,Kuna machungu ya kupita kifani pamoja na vifo, amesema Kamishna huyo wa Umoja wa Mataifa akihutubia nchi wanachama wa Baraza hilo sambamba na kuelezea uharibifu mkubwa uliotokana na miezi minane ya vita kwenye eneo hilo.

Halikadhalika, kuna wale waliokatwa viungo au kuuawa kutokana na mashambulizi hayo kutoka kwa Israeli na kwamba Bwana Türk amesema tangu jeshi hilo liimarishe operesheni za ushambulizi Rafah mapema mwezi Mei, takribani waisraeli milioni moja wamelazimika tena kuhama, na kusababisha mgao wa misaada ya kiutu kuwa ya shida.

Kuzuia kwa makusudi kusambaza misaada ya kiutu kumeendelea na Israeli inaendelea kuwashikilia maelfu ya wapalestina. Hii lazima ikome,” amesema Bwana Kamishna Mkuu huyo wa Haki za Binadamu huku akisimulia mazingira dhalili wanamoishi raia huko Deir Al-Balah, wamelundikana na huduma za kujisafi hakuna kwani kwa siku mtu mmoja anapatiwa chini ya lita moja ya maji.

Akigusia pia Ukingo wa Magharibi ambako nako ghasia za Gaza zimeenea hadi huko, bwana Türk ameonya pia kuzidi kuzorota kwa hali ya kibinadamu kwenye eneo hilo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa na Israeli, huku mashambulizi dhidi ya wapalestina yakiongezeka, vile vile kulengwa kwa askari wa Israeli.

Hadi kufikia Juni 15 mwaka huu wapalestina 528, kati yao 133 ni watoto, wameuawa na jeshi la Israeli au walowezi wa kiisraeli tangu Oktoba mwaka jana, na katika matukio mengi hoja ya mauaji kiholela imeendelea kushika kasi.

Katika kipindi hicho hicho, Waisraeli 23 wameuawa Ukingo wa Magharibi na pia Israeli kufuatia mashambulizi kutoka kwa wapalestina, ambapo kati yao hao, wanane ni wanajeshi.

Ikihusiana na mzozo wa Gaza, Kamishna Mkuu huyo wa Haki za Binadamu ameelezea hofu yake kubwa juu ya uwezekano wa kuzuka kwa vita kubwa kati ya Lebanon na Israeli.

Kuendelea kwa mashambulizi ya maroketi na mapigano kwenye mpaka wa pande mbili hizo kumesababisha vifo vya watu 401 Lebanon, wakiwemo madaktari na waandish iwa habari, amesema Bwana Türk, huku zaidi ya watu 90,000 wakiwa wamefurushwa makwao nchini Lebanon.

Nchini Israeli, takribani watu 60,000 wamelazimika kukimbia makazi yao na wengine 25 wameuawa, maelfu ya majengo yameharibiwa.

Katika tathmini yake ya madhara ya vita duniani, Kamishna huyo wa Haki za Binadamu ametumia takwimu akisema idadi ya raia waliouawa kwenye mizozo duniani mwaka jana iliongezeka kwa asilimia 72, takwimu zilizokusanywa na ofisi yake zimeonesha kuwa kiwango cha wanawake waliouawa mwaka 2023 kiliongezeka maradufu ilihali kiwango cha watoto waliouawa kiliongezeka mara tatu ikilinganishwa na 2022.

Akigeukia Ukraine, amesema operesheni za ardhini zinazofanywa na Urusi kwenye mkoa wa Kharkiv zimesambaratisha jamii nzima, wakazi wamejificha kwenye mahandaki bila umeme, huduma za maji na chakula cha kutosha wakiogopa mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa kwa kutumia vilipuzi na kuharibu eneo kubwa.

Bwana Türk pia amerejelea wito wa kulaani uharibifu wa miundobinu ya nishati ambao umekwamisha kwa asilimia 68 uwezo wa Ukraine wa kuzalisha nishati ya umeme.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *