Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kesi ya Mauaji ya Alphonce Mawazo Yapigwa Kalenda

Na Costantine James,Geita

Kesi ya mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Geita,Hayati Alphonce Mawazo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa upya hadi Juni 20, 2024 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Geita.

Kesi hiyo namba 56/2023 imeanza kusikilizwa upya Juni 18, 2024 chini ya Jaji Graffin Mwakapese lakini upande wa Jamhuri uliomba iahirishwe kutokana na kuwakilishwa na shahidi mmoja kati ya 20.

Upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na mawakili Godfrey Odupoy na Deodatho Dotto uliiambia mahakama kuwa shahidi huyo mmoja asingeweza kutoa maelezo ya kutosha katika kesi hiy na upande huo wa Jamuhuri ulieleza kusogezwa mbele kwa kesi hiyo kutawezesha kufika mahakamani kwa mashahidi wote na kesi itaweza kusikilizwa kwa mtiririko na mfululizo uliokamilika.

Jaji Mwakapese aliridhia ombi la upande wa Jamhuri ambapo alisoma maelezo ya awali na kuitaka Jamhuri kupeleka mahakamani hapo mashahidi wote Juni 20, 2024.

Upande wa utetezi ulikubaliana na ombi la Jamhuri na kuiomba mahakama kuhakikisha kesi hiyo ya jinai ya mauaji ya kukusudia isikilizwe na imalizike ndani ya kikao kilichopangwa,mpaka sasa kesi hiyo inahusisha washitakiwa wanne ambao ni Alfan Alpolinary (Kyaluboto) Apafula Zacharia (Mapinda), Hashimu Sharifu (Issa) na Kukulinda Bwire (Richard Bwire).

Mshitakiwa Alfan aliwakilishwa na wakili Rukia Marandu, mshitakiwa Mapinda aliwakilishwa na Yisambi Siwale, mshitakiwa Hashimu aliwakilishwa na Costantine Ramadhani huku Bwire akiwakilishwa na Beatrice Mgeni.

Washitakiwa wanadaiwa kumuua kwa kukusudia Alphonce Mawazo Novemba 14, 2015 siku chache baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na Desemba 24, 2020 Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ndogo ya Geita iliwahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa wanne

 baada ya kukutwa na hatia.

Washitakiwa walikata rufaa kwenda Mahakama Kuu Masijala ndogo ya Mwanza ambapo hukumu ya kesi hiyo ilifutwa na kuamuru kesi ianze kusikiliza upya kuanzia hatua za mahakama ngazi ya chini uamuzi wa Mahakama Kuu Masijala ndogo ya ulitokana na kukiukwa kwa kifungu cha 246 (02) cha sheria ya makosa ya jinai na kusababisha maamuzi ya mahakama ngazi ya chini kuwa batili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *