Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Korea  na Urusi ni Kutoshindwa na Kudumu

Rais wa Russia Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamekubaliana kuimarisha uhusiano kati ya mataifa yao, wakati wa mkutano wao katika siku ya kwanza ya ziara ya Putin mjini Pyongyang Jumatano ya leo Juni 19,2024.

Putin amefanya ziara yake ya kwanza Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka 24 iliyopita akiahidi kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiusalama na taifa hilo lililotengwa lenye silaha za nyuklia na kuliunga mkono dhidi ya Marekani.

Mkutano kati ya viongozi hao wawili unaonyesha kutoshindwa na kudumu kwa urafiki kati ya Korea Kaskazini na Russia, kulingana na shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini(KCNA).

Uhusiano wa Korea Kaskazini na Russia umeimarika “kama ngome imara ya kimkakati kwa kulinda sheria ya kimataifa, amani na usalama na kichocheo kwa kuharakakisha ujenzi wa ulimwengu wenye misimamo tofauti,” KCNA limesema.

Maafisa mjini Washington na Seoul wanasema Korea Kaskazini iliipa silaha Russia kuisaidia katika vita nchini Ukraine.

Moscow na Pyongyang zilikanusha kupeana silaha lakini zimeapa kuimarisha uhusiano wa kijeshi yakiwemo mazoezi ya pamoja kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *