Faida za Karafuu

Karafuu ni kiungo maarufu kinachotumika duniani kote, haswa bara la Asia; Karafuu hutengeneza msingi wa mapishi kwenye nyingi za Asia.

Karafuu ni kikonyo kilichokauka cha ua kutoka kwenye mti wa mkarafuu, kwa jina la kitaalamu huitwa Syzygium aromaticum. Mti huu upo kwenye familia ya miti iitwayo  Myrtaceae

Cloves (spice) and wooden spoon close-up food background


Karafuu imekuwa ikitumika kwa maelfu ya miaka nchini India na China si kama kiungo na kiongeza ladha kwenye chakula lakini pia kama dawa kwa matatizo mengi. 

Na hizi ndio faida za Karafuu.

Mmeng’enyo Bora: Karafuu  zinaweza kuimarisha mmeng’enyo kwa kuamsha uzalishwaji wa vimeng’enyi.   Karafuu pia ni nzuri kwa kupunguza gesi tumboni, tumbo kuvurugika (gastric irritability), kuvimbirwa, na kichefuchefu. Karafuu zinaweza kupikwa, kusagwa, au kuliwa pamoja na asali kwa afueni ya matatizo ya mmeng’enyo wa chakula.

Kuzuia Bacteria:Karafuu imekuwa ikizungumzwa na wengi kwa sifa zake za kuzuia bacteria dhidi ya vimelea viletavyo magonjwa kwa binadamu. Bidhaa/vitu vitokanavyo na karafuu vimetosha kabisa kuua vimelea vya magonjwa. Zalisho llitokanalo na karafuu pia ni muhimu dhidi ya bakteria waenezao ugonjwa wa kipindupindu. 

Kuzuia Kansa:Karafuu imekuwa muhimu kwenye jamii ya madawa kwa sifa zake za kuzuia kansa(carcinogenic properties). Utafiti uliochapwa kwenye jarida la Oxford Journal: Carcinogenesis imeonyesha kwamba karafuu zinaweza kusaidia kudhibiti kansa ya mapafu kwenye hatua za mwanzo. 

Ulinzi wa Ini :Karafuu zina kiasi kikubwa cha viondosha sumu, ambavyo ni muhimu kwa kulinda viungo vya mwili dhidi ya sumu huru (free radicals), hasa Ini.

#Chanzo: Afya Kweli.



Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *