Na Saulo Stephen – Singida.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wamepewa siku saba kuhakikisha wanarejesha Fedha zaidi ya shilingi Milioni 6 zilizokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato na kutowasilishwa katika account za benki ya Halmashauri hiyo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Omari Dendego wakati akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi mkuu wa Serikali (CAG).

Dendego amesema kuwa haiwezekani hoja ya shilingi milioni 6 kuwepo wakati ,katika Halmashauri hoyo ili hali wahusika wapo hivyo ni lazima fedha hiyo ilipwe ili kuondoa hoja hizo.
Aidha ameiagiza ofisi ya Utumishi katika Halmashauri hiyo kuwachukulia hatua watumishi wanaodaiwa fedha hizo kiasi cha Shilingi milioni 6 ili kukomesha tabia kama hiyo kwa watumishi wengine ndani ya mkoa wa Singida.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya singida akiwemo mkuu wa wilaya hiyo Godwin Gondwe pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Elia Digha Mlangi.