DRC YATAKA TIMU ZA ULAYA KUSITISHA MIKATABA YA VISIT RWANDA

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imevitaka vilabu vya Arsenal FC, PSG na Bayern Munich kusitisha mikataba yao ya matangazo ya Visit Rwanda, ikidai Rwanda inawaunga mkono na waasi wa M23.

Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo, Therese Kayikwamba imekosoa mpango huo wa matangazo wakati Taifa hilo likikabiliwa na vita katika eneo la Mashariki ambavyo vimesababisha zaidi ya watu 500,000 kuyahama makazi yao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo, Therese Kayikwamba Wagner.

Kupitia barua iliyoandikwa na Therese kwa timu ya Arsenal, Waziri huyo alisema uhalifu wa Rwanda katika mzozo huo hauna shaka baada ya UN kusema wanajeshi 4,000 wa nchi hiyo wapo DRC.

Amesisitiza kuwa mkataba wa Visit Rwanda huenda ukawa unachota fedha kutoka kwa madini haramu yanayopitishwa kinyemela kuvuka mpaka wa DRC na kuuzwa Rwanda kisha kupelekwa nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *