LENGO LA DRC NI KUMPINDUA KAGAME – RWANDA

Rwanda imekanusha taarifa iliyodai
kutolewa na Mkutano wa wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu uhusika wake na machafuko yanayoendelea DRC, huku ikisema Taifa hilo linalenga kumpindua Rais Paul Kagame.

Madai hayo yametolewa hii leo Februari 2, 2025 na Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda kupitia andiko lililochapishwa katika ukurasa wake wa X zamani Twitter.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe.

Chapisho hili linaeleza kuwa, “Rwanda inakana shutuma dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF), iliyotolewa katika taarifa ya Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Januari 31, 2025.”

Taarifa hiyo imezidi kueleza kuwa, RDF inatetea mipaka ya Rwanda dhidi ya vitisho na inalinda raia, haishambulii raia. SADC imetuma kikosi cha mashambulizi, SAMIDRC, kusaidia vita vya Serikali ya DRC dhidi ya watu wake wenyewe – M23 na wanachama wa jumuiya yao – wengi wao wamekimbilia kama wakimbizi nchini Rwanda na katika kanda nzima.”

Aidha, Wizara hiyo ya Mambo ya nje ya Rwanda inaeleza kwamba, “Serikali ya DRC pia ina nia ya kushambulia Rwanda na kupindua serikali yake, kama ilivyosemwa mara kwa mara na hadharani na Rais Tshisekedi.”

Hata hivyo, Rwanda imejinasibu kupitia ambatanisho la barua yake kuwa imekuwa ikitetea suluhu ya kisiasa inayotokana na mzozo unaoendelea kwa ustawi wa amani kama mapendekezo ya mkutano wa kilele wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC ulivyoainisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *