Baraza la Madaktari na Madaktari wa Meno nchini Kenya (KMPDC) limemfutia usajili Bw David Nyawade Onyango, ambaye amekuwa akijifanya daktari kumbe ni Daktari feki ambaye hana taaluma ya kuhudumu kwenye hopsitali.
Nyawade amefanya kazi ya Udaktari kwa miaka 16 katika sekta hiyo.
Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na msako mkali dhidi ya watu wanaojifanya wataalam wa afya kumbe hawana utaalumu wa mambo hayo.