Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo.

Pia Rais Samia amepokea zawadi ya Bendera (Pennant) ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kama kumbukumbu na zawadi hiyo amepewa na Rais wa Shirikisho hilo Dkt. Patrice Motsepe.

Mbali na hivyo Rais CAF, Patrice Motsepe lep pia aliongea na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema Msimu ujao timu 24 zitashiriki kwenye michuano ya African Football League na timu hizo zitapatikana kupitia ranki za CAF pamoja na mafanikio yake katika ligi za nyumbani.