Davido kukishitaki kituo cha habari Kenya

Staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido ameachia taarifa ya wazi kuhusu tuhuma za uongo zilizoandikwa na kituo kimoja cha habari Nchini Kenya kuwa msanii huyo alikamtwa uwanja wa Ndege akiwa na Dawa za Kulevya.

Kupitia taarifa yake aliyoiachia muda mchache uliopita, Davido ameweka wazi kuwasiliana na mwanasheria wake na kukichukulia hatua kituo hicho cha habari kwa kusambaza taarifa za uongo juu yake.

Taarifa ya Davido kukamatwa na Dawa za Kulevya ilisambaa siku ya jana Aprili mosi, na baada ya muda Ofisi ya mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini Kenya (DCI), ilikanusha taarifa hizo ambazo zilizosambaa mitandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *