NA SAADA ALMAS
Umoja wa maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda katika kata ya luguru wilayani Itilima mkoani Simiyu wamejitokeza kuchangia damu kwa hiyari na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa katika hospitali ya rufaa mkoa huo ili kuendelea kuokoa maisha ya wahitaji wa damu salama ambapo wengi wa wahitaji hao wakiwa ni maafisahao ambao wamekumbwa na changamoto mbalimbali za ajali za barabarani.
Akizungumza katika zoezi hilo Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dokta Athanas Ngambakubi amesema kuwa hospitali hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa kutoka hospitali za mkoa mzima hivyo mahitaji yanakuwa makubwa kiasi kwamba yanakuwa hayakidhi kuhudumia wagonjwa wote
“ndani ya wiki moja tunatumia unit 60 za damu ambapo kwa mwaka unit 700 zinahitajika lakini mahitaji ya damu hususan kwa akina mama wanaojifungua na majeruhi wa ajali yanakuwa hayatoshi kwa sababu tunategemewa na hospitali na vituo vyote vya afya ’’amesema ngambakubi
Sambamba na hilo amesema kuwa kuna kipindi wanakuwa na uhitaji wa damu lakini grupu la damu hasa o negativu huwa ngum kupatikana hivyo wanalazimika kwenda mikoa jirani kutafuta damu na kwa kuwa wanapokea wagonjwa wengine wakiwa katika hali mbaya sana damu ikikosekana kwa wakati hupoteza maisha
‘’katika mkoa wetu matukio ya ajali yanayohusisha kichwa na kupoteza fahamu tunayapokea na wastani ni wagonjwa watatu hadi wanne kwa wiki huku na tukimpima kwa wenye majeraha ya kichwa tunakuta damu imeshavujia kwenye ubongo sasa tukimpa vipimo ikaonekana anahitaji damu hasa grup o- huwa tunawapa rufaa kuwapeleka hospitali ya kanda ya bugando ‘’ameongeza ngambakubi
Kamanda wa polisi mkoani simiyu Edith Swebe amesema kuwa moja ya mkakati uliopangwa na jeshi hilo ni kuondoa kabisa ajali mkoani humo hasa katika kuelekea msimu wa sikukuu na hiyo ndiyo sababu wamejiunga pamoja na maafisa hao kufika hospitali hapo kujionea hali ilivyo kwa waathirika wa ajali na hatimaye wawe mabalozi wa madereva wengine wasio fuata sheria
‘’kutokutii sheria za usalama barabarani kunagharimu maisha na hata kukupa ulemavu wa kudumu ndiyo maana tunatoa elimu na leo tumekuja nanyi ili mjionee kwa vitendo madhara ya kutotii sheria nitoe rai kwenu jifunzeni sheria na mzifahamu ,tafuteni leseni na ikiwezekana muwe ikiwezekana mkate bima za afya na bima za vyombo vyenu ‘’ amesema Swebe
kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani simiyu Amos Kadonya amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2025 wanampango wa kusajili vijiwe vyote vya bodaboda kuweka uongozi kati yao ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuchanga walau elfu moja kila siku ili iwasaidie kupata leseni na mahitaji yao ya kofia ngumu na viatu ili kupunguza madhara ya ajali
‘’kama mkoa tumejipanga kusajili vijiwe vyote hadi 2025 na vitakuwa na viongozi ambao tutausimamia kwa karibu ili atakaye jiunga nao na bila kuvaa kofia ngumu wanatakiwa kumfukuza wao wenyewe’’amesema Kadonya
Aidha mwenyekiti wa umoja huo Mwanjale magembe amesema kuwa kufika kwao katikahospitali hiyo kumewaa picha ya namna gani wenzao wanateseka kutokana na aji za barabarani hivyo anatoa rai kwa madereva wote kutii sharia ‘’tumekuja kujifunza kwa vitendo na tumeona ni namna gani ndugu zetu wanatesekakwa hiyo tunajifunza kuwa mwendo kasi siyo dili na tunatakiwa tuvae kofia ngumu na tutii sheria za barabarani’..’