Bayern Munich yalala 2-1 mbele ya Manchester City

FC Bayern Munich imekubali kibano cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester City, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa mchana wa leo Tokyo, Japan kwenye uwanja wa Taifa wa Japan.

Mabao ya Manchester City katika mchezo wa leo yamefungwa na James McAtee Dakika ya 21 na Aymeric Laporte dakika ya 86, huku bao pekee la Bayern Munich likifungwa na Mathys Tel dakika ya 81.

Hii ni mechi ya pili ya kirafiki kwa Bayern, ya kwanza walipata ushindi mnono wa mabao 27-0 dhidi ya Rottach Egern, Kwa upande wa City hii nayo ni mechi ya pili kwao baada ya kwanza kupata ushindi wa 5-3 dhidi ya Yokohama Marinos.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *