Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Afrika kuwa na uchumi imara ifikapo 2063

Rais Samia Suluhu Hassan Amewataka Viongozi Wa Afrika Kujitathmini Na Kuamua Ni Kwa Namna Gani Wataweza Kutumia Uwezo Na Rasilimali Za Afrika Kujikwamua Kiuchumi, Ili Kufikia Malengo Ya Ajenda Ya Kuitoa Afrika Ilipo Na Kuifanya Kuwa Na Uchumi Imara Kufikia 2063 ‘Transforming Afrika Into The Global Power House Of The Future.’

Rais Samia Ameyasema Hayo Leo Julai 26, 2023 Katika Mkutano Wa Kimataifa Wa Wakuu Wa Nchi Za Afrika Kuhusu ‘Rasilimali Watu’ Katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam Ambapo Amesema Ni Muda Muafaka Sasa Viongozi Wa Afrika Kulizungumzia Hili Kutokana Na Faida Ya Vijana Barani Afrika.

Samia Amenukuu Takwimu Za Jukwaa La Uchumi La Dunia ‘World Economic Forum’
“Takwimu Zinaeleza Ifikapo 2050 Afrika Itatoa Nchi 10 Zenye Idadi Kubwa Za Vijana Duniani.” Amesema Samia Na Kuongeza

“Ifikapo 2030 Afrika Itakuwa Na Asilimia 42 Ya Vijana Wote Duniani Wenye Umri Chini Ya Miaka 25.”

Pia Ameorodhesha Mambo Kadhaa Ya Kuzingatia Ili Kuwa Na Mageuzi Ya Kiuchumi Kupitia Rasilimali Watu.

Mambo Aliyoyataja Ni Pamoja Na Uzazi Wa Mpango, Utoaji Wa Elimu Bora, Uimarishaji Wa Sekta Ya Afya Na Lishe Kwa Watoto Pia Kuwekeza Katika Sekta Nyingine Ikiwemo Miundombinu Ya Usafirishaji, Nishati, Teknolojia Na Nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *