Asilimia 75 ya watu wenye kifafa hupelekwa kwa waganga wa kienyeji badala ya hospitali

Chama cha Wanasayansi wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu Tanzania (TNA), kimesema asilimia 75 ya watu wenye kifafa hupelekwa kwanza kwa waganga wa kienyeji na viongozi wa kiroho badala ya hospitali hali inayopelekea ugumu wakati wa kuudhibiti.


Mwenyekiti wa TNA, Profesa William Matuja amesema idadi kubwa ya watu nchini wana imani potofu kuhusu kifafa, ambapo zaidi ya asilimia 36 bado wanaamini ugonjwa wa kifafa unatokana na nguvu za giza ikiwemo mapepo wachafu.


Aidha, amefafanua kuwa asilimia 26 ya wagonjwa wa kifafa wana matatizo ya kimwili kutokana na mshtuko wa moyo ambao haujatibiwa ikiwa ni pamoja na makovu mwilini, majeraha ya moto, mikazo, kuteguka kwa viungo hasa mabega, kuumia kichwa na vifo vya mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *