Kijana atobolewa macho na kulawitiwa  kabla ya kuuawa.

Kijana Mmoja aliyefahamika kwa jina la Henry Tumaini Lekule (34) amefariki dunia Mkoani Arusha kwa kujeruhiwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake kichwani, Pamoja na kutobolewa macho huku pia ikielezwa alilawitiwa kabla ya kuuawa.

Tukio hilo linahusishwa na Wivu wa kimapenzi, ikidaiwa Henri aliwahi kumfumania mkewe ambaye alimshawishi kuhama kwao na kuhamia ukweni, huku wakijaaliwa Watoto wawili kati ya watatu aliozaa mkewe.

Kulingana na Familia ya Mzee Tumaini Lekule amesema tukio hilo limetokea usiku wa jumapili ya kuamkia jumatatu ya Februari 12, 2024, eneo la Block D, Njiro jijini Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *