Wachezaji wa timu ya soka ya Ivory Coast wazawadiwa pesa na nyumba za kifahari

Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast na kocha wao Emerse Fae wamezawadiwa pesa na nyumba za kifahari katika hafla iliyosimamiwa na Rais wa nchi hiyo katika kusherekea ushindi wao wa fainali ya kombe la mataifa barani Afrika.

Kila mchezaji amepewa milioni 50 za sarafu ya CFA na nyumba ya kifahari yenye thamani sawa na pesa hizo.


Kocha Fae amepewa milioni 100 za sarafu ya CFA kwa kuongoza vizuri wachezaji wake baada ya kuchukua nafasi ya kocha mkuu aliyetimliwa Jean Louis Gasset katikati ya mashindano kufuatia kipigo kibaya cha mabao 4-0 dhidi ya Equatorial Guinea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *