Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Aondolewa jinsia ya kike na kubaki na ya kiume

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imefanikiwa kufanya upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike kutoka kwenye korodani ya mgonjwa wa jinsia mbili mwenye muonekano wa jinsia ya kiume. Upasuaji huo umefaywa na jopo la madaktari kutoka hospitali hiyo, na limeongozwa na Daktari Bingwa wa upasuaji wa jumla na mfumo wa mkojo, Dr Hussein Msuma pamoja na wasaidizi wake ,Dr Hamis Mbarouk,Mr Curtius Mbalamula, Mr Mkati na Sr Shani Maupa.

Upasuaji huo umefanyika kwa mara ya kwanza katika hospitali hiyo na kwa mara ya kwanza kwa hospitali za rufaa zilizopo Tanzania. Kufanyika kwa upasuaji huu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temke ni moja ya mafanikio makubwa katika Sekta ya Afya Tanzania.
Akizungumza baada ya upasuaji kufanyika na kufanya vipimo vya sampuli zilizo tolewa katika upasuaji, Dr Hussen Msuma amesema kuwa ni kweli Mgonjwa alifika Hospitalini akiwa na muonekano wa jinsia ya Kiume lakini ana maumbile ya ndani ya aina mbili yaani umbile la kike na la kiume, hivyo kupelekea upasuaji huu.

Kwa lugha ya kitaalamu huu upasuaji unaitwa scrotal hystero-salpingo-oophorectomy na kwa lugha rahisi ni upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike kutoka kwenye korodani ya mgonjwa wa jinsia mbili mwenye muonekano wa jinsia ya kiume. Ugonjwa huu unatokana na changamoto wa ukuaji wa kijinsia (ovotesticular DSD), ni ugonjwa nadra na adimu sana kutokea ambapo binaadamu huzaliwa na viungo vya ndani vya uzazi (gonadi) za jinsia zote (ovari za kike na korodani za kiume).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *