Unaweza kujiuliza ni nani anahusika kumpaka make-up nguli wa soko #DavidBeckham? Jibu ni kuwa anayempaka make up, staa huyo ni binti yake Harper Seven Beckham.
Hivi karibuni Harper alidhihilisha hilo kupitia video fupi iliyowekwa na Beckham katika ukurasa wake wa Instagram ambapo walikuwa wakijiandaa kwenda kwenye maonyesho ya mitindo ya #ParisFashionWeek yaliyofanyika Mjini Paris- Ufaransa. Na maonyesho hayo yalihitimishwa Septemba 30.