Amuua kwa sumu ya panya baba wa mpenzi wake



Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia Mitedi Mwambughi (63) kwa tuhuma za kumuua kijana anayedaiwa kuwa ni hawara wa binti yake kwa kumnywesha sumu inayodhaniwa kuwa ni ya kuulia panya.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumnywesha sumu, Christopher Mwamengo (23), kwa kumweka kinyumba binti yake huyo (19), wakati akijisubiri kujiunga na chuo baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka huu.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Rashid Ngonyani, amesema tukio hilo limetokea Septemba 13 mwaka huu katika Kijiji cha Ikonya, Kata ya Bara, Wilaya ya Mbozi.

Ngonyani amesema inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alichukua uamuzi wa kumywesha sumu kijana huyo kama njia ya kulipiza kisasi baada ya kumtorosha binti yake na kumweka kinyumba kwa zaidi ya siku mbili bila ridhaa yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *