Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Saba waingia 18 za Mchengerwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI] Mohamed Mchengerwa, amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwachukulia hatua za kinidhamu Watumishi saba wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo kuzorotesha utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za Halmashauri hiyo.

Mchengewa amechukua uamuzi huo wakati wa ziara katika Wilaya ya Liwale ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mchengerwa ameelekeza hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa mujibu wa Kanuni ya 42 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022 inayoainisha kuwashusha vyeo, kukatwa mshahara kwa asilimia 15 kwa muda usiopungua miaka 3 pamoja na kufukuzwa kazi iwapo watabainika kufanya makosa hayo.

Waziri Mchengerwa pia ameelekeza kuanzia sasa Maafisa wote wenye kesi za rushwa na ubadhilifu wasihamishwe vituo vyao vya kazi mpaka mashauri yao yanapokamilika.

“Afisa yeyote mwenye kesi ya uhujumu uchumi au ubadhilifu wakati kesi yake ikiendelea ataendelea kuchunguzwa mienendo yake na hukumu yake ikitoka hatopewa tena jukumu la Ukuu wa Idara au Kitengo hadi mienendo yake itakaporidhisha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *