Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Aliyetenguliwa na Mchengerwa atenguliwa na Samia

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Busega, Veronica Sayore.

Taarifa za kutenguliwa kwa Sayore, zimetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus ambaye pia ameeleza mabadiliko kadhaa yaliyofanywa na Rais Samia.

Uamuzi wa Rais Samia kutengua uteuzi wa Sayore, unakuja wiki kadhaa tangu Waziri Mohamed Mchengerwa wa TAMISEMI kumsimamisha mkurugenzi huyo kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

Mchengerewa alimsimamisha Sayore tangu Septemba 22, 2023 na kueleza kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kuhusu utendaji kazi usioridhisha, kutokuwa na ushirikiano na viongozi wenzake pamoja na kutowashirikisha watendaji katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *