Aliuwawa na Kundi la Hamas Oktoba 7 baada ya kutekwa

Waziri wa Mambo ya Nje, January Makamba amesema Serikali ya Israel imeijulisha Tanzania kuwa Mtanzania Joshua Mollel aliuawa na kundi la Hamas mara tu baada ya kutekwa Oktoba 7 mwaka huu.

Joshua alitekwa pamoja na Clemence Mtenga ambaye naye aliuawa na mwili wake ulizikwa kijijini kwao Rombo mkoani Kilimanjaro Novemba 28 mwaka huu.

Makamba amesema “Nimeongea na Mzee Mollel, Baba mzazi wa Joshua, kuhusu ujumbe huo wa Serikali ya Israel, tunaendelea na mpango wa awali wa kuwapeleka Mzee Mollel na Mwanafamilia mwingine pamoja na Afisa wa Serikali nchini Israel, kuungana na Balozi wetu na Maafisa waliopo huko, kukutana na kuzungumza na mamlaka za Nchi hiyo ili kupata taarifa za ziada, kwa ridhaa ya Familia, na itakapobidi, tutatoa taarifa za ziada katika siku zijazo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *