Mtuhumiwa anayedaiwa kusababisha kifo cha Beatrice Minja kwa kumchoma visu mara 25, Lucas Tarimo amefariki dunia akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi wakati akiendelea na matibabu katika hospitali ya Huruma iliyopo Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.
Daktari kiongozi wa Hospitali ya Huruma wilayani hapa, Daria Mushi amethibitisha kutokea kwa kifo chake ambapo amesema amefariki Januari Mosi, 2024 saa nne na nusu usiku.