Staa wa filamu kutoka Nigeria Tonto Dikeh, amejitokeza na kusema atamchangia rafiki yake, Iyabo Ojo pesa ili asiende jela baada ya Naira Marley kutaka fidia ya Naira Milioni 500 sawa na Tsh/=1,521,288,410.00 kutokana na machapisho ya mwanamama huyo.
Dikeh amesema hayo katika ukurasa wake wa Instagram hivi karibuni.
Utakumbuka tarehe 14 Desemba, 2023 Naira Marley alifungua kesi dhidi ya Iyabo, ambapo
ametishia kuchukua hatua za kisheria ambazo zinaweza kugharimu Naira Milioni 500 sawa na Tsh/=1,521,288,410.00 kama fidia isipokuwa mwigizaji huyo ataomba msamaha wa umma, kwa kile alihodai alimkashifu kwa kuandika habari za uwongo juu yake kwenye ukurasa wake wa Instagram.